Rais Xi akagua mkoa wa Qinghai, kaskazini magharibi mwa China
2021-06-07 22:25:34| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ameanza ziara ya ukaguzi mkoani Qinghai, kaskazini magharibi mwa China.

Katika mji mkuu Xining, rais Xi alitembelea kampuni inayotengeneza zulia na kufahamishwa jinsi ya kutumia vizuri malighafi ya eneo hilo na kutoa mawazo mapya ya kiubunifu ili kuongeza nguvu ya ushindani ya bidhaa zake, kutoa nafasi za ajira na kuongeza mapato ya watu.

Xi pia alitembelea eneo la makazi mjini Xining na kufahamishwa kuhusu juhudi za kuimarisha ujenzi wa Chama, kuboresha utawala mashinani na kuhimiza umoja na maendeleo ya kikabila.