Bangladesh yaidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya SINOVAC ya China
2021-06-07 09:08:42| CRI

Mamlaka ya dawa Bangladesh imeidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na kampuni ya SINOVAC ya China nchini Bangladesh.

Hii ni chanjo ya pili ya China iliyopewa idhini ya matumizi ya dharura nchini Bangladesh, baada ya nchi hiyo kutoa kibali kwa chanjo ya Sinopharm ya China mwishoni mwa mwezi Aprili. Chanjo ya Sinopharm ilianza kutolewa nchini humo mwezi Mei.

Bangladesh ilianza zoezi la utoaji chanjo mwishoni mwa mwezi Januari. Kutokana na ripoti iliyotangazwa na wizara ya afya ya Bangladesh, hadi sasa nchi hiyo imetoa dozi milioni 9 za chanjo ya COVID-19 kwa watu wake.