Nchi 18 zachaguliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Uchumi na Jamii la UN kwa kipindi cha miaka mitatu
2021-06-08 09:00:02| CRI

Mwenyekiti wa baraza mkuu la Umoja wa mataifa Bw. Volkan Bozkir amesema nchi 18 zimechaguliwa kuwa wajumbe wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwezi Januari mwaka kesho.

Amezitaja nchi hizo kuwa ni Cote d’Ivoire, Eswatini, Mauritius, Tanzania, na Tunisia kutoka Afrika, Afghanistan, India, Kazakhstan na Oman kutoka eneo la Asia-Pasifiki, Croatia na Jamhuri ya Czech kutoka Ulaya Mashariki, Belize, Chile na Peru kutoka eneo la Latin Amerika na Caribbean, pamoja na Ubegiji, Canada, Italia na Marekani.

Baraza hilo lina wajumbe 54 ambao huchaguliwa kila mwaka kwa vipindi vya miaka mitatu mitatu, na wajumbe hao wanagawanywa kwa mujibu wa uwakilishi wa kijiografia.