Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa apigwa kofi kwenye ziara yake wilayani Drome
2021-06-09 08:25:32| CRI

Watu wawili wamekamatwa baada ya rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kupigwa kofi kwenye ziara yake wilayani Drome, kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Video iliyotolewa kwenye chaneli ya habari ya BFM TV, inaonesha rais Macron akielekea kwenye umati wa watu waliokuwa wakimshangilia na kumsalimia mtu mmoja, ambaye alimpiga kofi.

Watu wawili walikamatwa baadaye kwa tuhuma za kutumia mabavu dhidi ya ofisa wa serikali.