Rais wa China aagiza mashirika ya shina ya CPC yawahudumia vizuri watu
2021-06-09 08:15:08| cri

Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesisitiza kuwa mashirika ya shina ya chama hicho yanapaswa kutoa huduma nzuri kwa watu.

Rais Xi ameyasema hayo wakati alipotembelea makazi ya watu mjini Xining mkoani Qinghai kaskazini magharibi mwa China.
Rais Xi amesema kila mara anapofanya ukaguzi, anatembelea makazi ya watu vijijini na mijini ili kuona jinsi maisha ya watu yanavyoendelea. Amesisitiza kuwa mashirika ya shina ya CPC yanatakiwa kutoa huduma bora za jamii katika nyanja zote.