Benki ya dunia yarekebisha makadirio ya ongezeko la uchumi wa China kuwa asilimia 8.5 kwa mwaka huu
2021-06-09 08:45:23| CRI

Ripoti kuhusu makadirio ya uchumi iliyotolewa jana na benki ya dunia inaonyesha kuwa uchumi wa China uko kwenye mwelekeo wa kukua kwa asilimia 8.5 kwa mwaka 2021, ikiwa ni juu kwa asilimia 0.6 ikilinganishwa na makadirio yaliyotolewa awali.

Uwezo wa China kudhibiti janga la COVID-19 kwa haraka, uungaji mkono wa kisera, pamoja na kuongezeka kwa biashara duniani, vimetajwa kuwa na mchango mkubwa kwenye kuhimiza ongezeko la uchumi wa China.

Wakati huo huo ongezeko la uchumi wa dunia kwa mwaka huu limekadiriwa kuwa asilimia 5.6, likiwa ni asilimia 1.5 zaidi kuliko makadirio ya awali, na hii ni kutokana na ongezeko kubwa kwenye nchi zenye uchumi mkubwa.

Hata hivyo licha ya ufufukaji huo, ongezeko la uchumi wa dunia litakuwa chini kwa asilimia 2 kuliko lilivyokadiriwa kabla ya janga la Corona.