China yapanga kuanzisha mpango wa kurejesha sampuli ya Mars ifikapo mwaka 2030
2021-06-14 10:55:51| Cri

Msemaji wa Idara ya taifa ya mambo ya anga ya juu ya China CNSA Xu Hongliang amesema, China inapanga kuanzisha mpango wa kurejesha sampuli ya Mars ifikapo mwaka 2030. Pia ametangaza kuwa mpango wa kwanza ya Mars ya Tianwen-1 imepata mafanikio.

Pia amesema katika historia ya maendeleo ya anga ya juu, China imeweka alama kwa kutekeleza hatua tatu za kuzunguka, kutua na kusafiri katika mpango mmoja, hali ambayo imeonesha kuwa China imekuwa nchi ya kiwango cha kwanza katika utafiti wa sayari.  Pia amesema China inapanga kuzindua mradi wa kukusanya sampuli kutoka kwenye sayari ndogo na kutafiti vimwondo katika mpango mmoja ifikapo mwaka 2025, na kutafiti mfumo wa mbali zaidi wa Jovian baada ya mwaka 2030.