Umoja wa Mataifa wasisitiza mshikamano na watu wenye ulemavu wa ngozi
2021-06-14 09:27:06| CRI

 

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza mshikamano na watu wenye ulemavu wa ngozi hapo jana, ambayo ilikuwa ni Siku ya Kimataifa ya Walemavu wa Ngozi.

Bw. Guterres amesema, kaulimbiu ya mwaka huu: “Nguvu Inayopita Changamoto Zote”, inaashiria uvumilivu, uimara na mafanikio ya watu wenye ulemavu wa ngozi katika dhana potofu ya kutowaelewa, kuwatenga na matumizi ya mabavu dhidi yao.

Habari nyingine zinasema, serikali ya Tanzania imeahidi kuwalinda kikamilifu watu wenye ulemavu wa ngozi kwa kuongeza ulinzi wao.

Akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Walemavu wa Ngozi Duniani hapo jana, naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulika na Watu wenye Ulemavu, Bi. Ummy Hamis Nderinanga amesema, watu wenye ulemavu wa ngozi wanapaswa kuwa salama kwa kuwa ulinzi wao umeendelea kupewa kipaumbele na serikali.

Amewataka wenzi wa maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali ili kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi.