Rais wa China ataka kazi ya uokoaji ifanyike baada ya bomba kuu la gesi kulipuka mkoani Hubei
2021-06-14 09:28:09| cri

 

 

Rais Xi Jinping wa China ameamuru juhudi zote zitumike katika kuwaokoa watu waliojeruhiwa baada ya mlipuko wa gesi kutokea katika mkoa wa Hubei, katikati ya China jana asubuhi.

Rais Xi amezitaka mamlaka husika kuzifariji familia za watu waliopoteza maisha katika tukio hilo na kufanya uchunguzi haraka.

Mlipuko wa gesi ulitokea majira ya saa 12:40 asubuhi kwa saa za China katika soko la umma mjini Shiyan na kusababisha vifo vya watu 12 na wengine 37 kujeruhiwa vibaya.

Naye waziri mkuu wa China, Li Keqiang, ametaka juhudi zifanyike kupanga kazi ya uokoaji, kuwatibu majeruhi na kupunguza idadi ya vifo. Pia ameamuru kutafuta chanzo cha ajali hiyo, kuhakikisha wajibikaji kamili kuendana na sheria na kanuni, na kutaka juhudi zifanyike kuimarisha usimamizi katika maeneo muhimu na kutambua uwezekano wa hatari ili kuzuia ajali mbaya kutokea.