Naftali Bennett aapishwa kuwa waziri mkuu wa Israel
2021-06-14 09:26:41| CRI

 

 

Waziri mkuu mteule wa Isarel Naftali Bennett ambaye ni kiongozi wa Chama cha Umoja wa Mrengo wa Kulia na mawaziri wa serikali mpya ya nchi hiyo wameapishwa jana usiku.

Vyama nane vilivyounda serikali mpya ni pamoja na Chama cha mrengo wa kushoto cha Kuwa na Mustakabali, Chama cha Umoja wa Mrengo wa Kulia, Chama cha Rangi za Bluu na Nyeupe, na Chama cha Umoja wa Kiarabu.

Kwenye mkutano wa kwanza wa serikali mpya, Bennett amesema serikali hiyo itajitahidi kuondoa migongano ya watu na kuifanya Israel kurejea kwenye hali ya kawaida.