Mkutano wa G7 wamalizika
2021-06-14 08:38:32| cri

Mkutano wa siku 3 wa Kundi la Nchi 7 (G7) umemalizika jana. Jumapili, ambapo Kundi hilo limeahidi kutoa dozi bilioni 1 za chanjo ya COVID-19 kwa dunia ili kuharakisha kumalizika kwa janga hilo.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Kundi hilo pia imesema, nchi wanachama wa Kundi hilo zitaongeza ushirikiano kujenga mfumo wa dharura wa kukabiliana na suala la afya duniani, na kujitahidi kufupisha muda wa uvumbuzi wa chanjo mpya uwe ndani ya siku 100.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ingawa ahadi ya kundi hilo ni sahihi, lakini jitihada zilizofanywa na kundi hilo kwenye mapambano dhidi ya janga la COVID-19 bado ni ndogo.