China yatoa mwongozo wa kujenga eneo la kielelezo la ustawi wa pamoja mkoani Zhejiang
2021-06-14 11:07:23| cri
Hivi karibuni, Baraza la Serikali la China limetoa mwongozo kuhusu kujenga eneo la kielelezo la ustawi wa pamoja mkoani Zhejiang.
Kulingana na mwongozo huo, ifikapo mwaka 2025, ujenzi huo unatarajiwa kupata mafanikio tele ambapo muundo wa jamii yenye tabaka kubwa la kati utakamilika kimsingi. Mkoa wa Zhejiang unatarajiwa kutimiza lengo la ustawi wa pamoja ifikapo mwaka 2035.
Katibu wa Kamati ya Chama cha CPC ya mkoa wa Zhejiang Yuan Jiajun amesema, uvumbuzi wa kisayansi na teknolojia ya kidijitali vinapaswa kutumiwa kuinua maendeleo ya uchumi na jamii yafikie kiwango cha juu zaidi, na vilevile kuboresha huduma za kijamii ili wananchi waweze kupata manufaa halisi kutokana na ustawi wa pamoja, na hivyo kuchochea msukumo mkubwa wa jamii kuelekea lengo la ustawi wa pamoja.