Macron: Kuendeleza uhusiano na China kunahitaji uwazi na heshima
2021-06-14 10:55:25| Cri

Baada ya Mkutano wa viongozi wa Kundi la G7 kumalizika jana mchana, rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema kundi la G7 halipaswi kuvutana na China, bali linahitaji kufanya juhudi za pamoja na China katika masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, biashara ya kimataifa na sera za maendeleo. Pia alisema China imewafanya mamilioni ya watu kuondokana na umaskini katika miaka miongo kadhaa iliyopita, pia amekiri tofauti zilizopo kati ya China na nchi za magharibi, akisisitiza kuwa kukuza uhusiano kiwenzi na ushirikiano na China kunahitaji uwazi na heshima, na kundi la nchi saba linatakiwa kukabiliana na tofauti moja kwa moja, wala si kuzidisha tofauti hizo kupita kiasi. Siku hiyo Rais Macron alipoulizwa kuhusu utafiti wa chanzo cha virusi alisisitiza kuwa, hivi sasa ni muhimu kufahamu chanzo cha virusi, lakini haipaswi kuamini kauli ya nchi moja. Utafiti wa chanzo cha virusi unapaswa kutegemea ukweli wa mambo, ushirikiano wa nchi zote, na kufanya utafiti chini ya uongozi wa Shirika la Afya Duniani WHO.