Rais Putin wa Russia asema NATO ni “mabaki ya Vita Baridi”
2021-06-15 10:25:00| CRI

Rais Vladimir Putin wa Russia hivi karibuni alipohojiwa na televisheni ya NBC ya Marekani, amesema “NATO ni mabaki ya Vita Baridi”, na kwamba haelewi kuna maana gani kubakiza matokeo haya ya Vita Baridi.

Akizungumiza luteka ya jeshi la Russia, Rais Putin amesema NATO inaendelea na upanuzi wake upande wa Mashariki, na kujenga miundombinu ya kijeshi kwenye maeneo yaliyo karibu na mpaka wa Russia. Lakini Russia kamwe haikuchukua hatua za kivamizi, na wala kutoa tishio kwa Marekani na Ulaya.

Rais Putin pia ameeleza wasiwasi wake kutokana na NATO kutangaza kuuchukulia mtandao wa Internet kuwa medani ya kivita na kupanga kufanya luteka ya kijeshi mtandaoni. Amesema Russia haitaki kuufanya mtandao uwe nyanja ya kijeshi, na inatarajia kushirikiana na Marekani katika kusukuma mbele mchakato wa usalama mtandaoni.