Maseneta tisa wa DRC waambukizwa Corona
2021-06-15 10:25:30| CRI

Spika wa Baraza la Seneti la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Modeste Bahati Lukwebo amethibitisha kuwa maseneta tisa wameambukizwa virusi vya Corona, na watu 38 kati ya wafanyakazi 358 wa baraza hilo waliofanyiwa vipimo vya COVID-19, wamekutwa na matokeo chanya.

Ijumaa iliyopita Rais Felix Tshisekedi wa DRC alisema serikali yake itatangaza hatua mpya za kudhibiti maambukizi katika siku kadhaa zijazo kufuatia nchi hiyo kushuhudia wimbi la tatu la mlipuko wa virusi hivyo. Pia alieleza nia ya kuingiza chanjo za China na Russia na kuhamasisha wananchi wajitokeze kupata chanjo ya COVID-19.