Magari ya kisasa ya umeme ya China yaongoza duniani
2021-06-15 10:25:54| CRI

Mkutano wa kilele wa sekta ya magari ya China uliofanyika kwa siku mbili mjini Chongqing, magharibi mwa China, ulifungwa Jumapili. Mkurugenzi wa Kitengo cha Kwanza cha Viwanda vya Utengenezaji wa Mashine katika Wizara ya Viwanda na Tehama Bw. Luo Junjie amesema, takwimu mpya zinaonesha kuwa magari ya umeme ya kisasa ya China yanaongoza duniani, na mauzo ya magari ya umeme nchini China yanachukua nafasi ya kwanza kote duniani kwa miaka sita mfululizo.