Iran yasema bado kuna masuala kadhaa ambayo hayajatatuliwa kkuhusu suala la nyuklia
2021-06-15 08:26:19| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Bw. Saeed Khatibzadeh amesema, mkutano wa pande husika za suala la nyuklia la Iran bado unaendelea mjini Vienna, Austria.

Bw. Khatibzadeh amesema, masuala ya kiufundi, kisheria na kiutawala bado yanaendelea kujadiliwa na kutatuliwa kwenye mkutano huo, na kuihimiza serikali ya sasa ya Marekani kuepuka vitendo vilivyofanywa na rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump.

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema, Iran itatimiza wajibu wake mara pande zote husika zikitimiza ahadi zao katika makubaliano ya suala hilo.