Katibu mkuu wa UM aihimiza G7 kutekeleza ahadi ya ufadhili kwenye suala la hali ya hewa
2021-06-15 10:27:36| cri

 

 

Kabitu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amezihimiza nchi zilizoendelea hasa Kundi la Nchi 7 (G7) zitekeleze ahadi zao za kutoa dola za kimarekani milioni 10 kila mwaka kwa nchi zinazoendelea ili kusisaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Pia katibu mkuu huyo amesisitiza kuwa ahadi hizo ni muhimu sana kwa kujenga uaminifu wa pande mbalimbali na kutimiza lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi lililofikiwa katika Makubaliano ya Paris.

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun amekubaliana na maoni ya Bw. Guterres, akisisitiza kuwa, kushindwa kwa nchi zilizoendelea kutekeleza ahadi zao kumeathiri vibaya utimizaji wa makubaliano ya Paris.