UM wasema ahadi ya G7 ya kutoa chanjo haiwezi kukidhi mahitaji ya sasa
2021-06-16 08:41:08| cri

Mkutano wa Kundi la Nchi 7 (G7) umemalizika jumapili, ambapo Kundi hilo limeahidi kutoa dozi bilioni 1 za chanjo ya COVID-19 kwa dunia kabla ya mwisho wa mwaka ujao. Lakini maafisa wa Shirika la Afya Duniani wanaona kuwa idadi hii ya chanjo “haitoshi sana”.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, ingawa ahadi ya Kundi hilo ni msaada mkubwa, lakini chanjo zaidi zinahitajika haraka. Amesema, hivi sasa, watu zaidi ya elfu 10 wanakufa kila siku kutokana na virusi vya Corona, na kwamba chanjo hizo zinahitajika sasa, na siyo mwakani.

Mjumbe maalum wa uratibu wa COVAX, Bw. Carl Bildt amesema, dozi zitakazotolewa na G7 ni kidogo sana, kwani dozi bilioni 11 za chanjo zinahitajika ili kutimiza lengo la kuwezesha asilimia 70 ya watu kupata chanjo kabla ya mkutano wa mwaka kesho wa kundi hilo.