Kiwango cha kutojua kusoma na kuandika mkoani Xinjiang kiko chini kuliko kiwango cha wastani kote nchini
2021-06-16 10:37:15| Cri

Kiwango cha kutojua kusoma na kuandika mkoani Xinjiang kiko chini kuliko kiwango cha wastani kote nchini_fororder_2a

Matokeo ya sensa ya kitaifa ya saba iliyotolewa hivi karibuni yameonesha kuwa, wastani wa muda wa kupata elimu kwa watu wenye umri wa miaka 15 na zaidi mkoani Xinjiang, umeongezeka kutoka miaka 9.27 ya mwaka 2010 hadi miaka 10.11 ya mwaka 2020, ukishika nafasi ya kumi kati ya mikoa yote 31 kote nchini.

Mwaka 2020, kiwango cha watu wasiojua kusoma na kuandika mkoani Xinjiang kilikuwa asilimia 2.66, ambacho ni chini kwa asilimia 0.01 kuliko kiwango cha kitaifa. Ikilinganishwa na sensa ya sita ya kitaifa ya mwaka 2010, idadi ya watu waliopata elimu ya chuo kikuu kati ya kila watu laki moja mkoani Xinjiang imeongezeka kutoka 10,635 hadi 16,536, ambayo ni kubwa zaidi kwa 1,069 kuliko kiwango cha wastani kote nchini.