China na Russia zawaalika washirika wao wa kimataifa kushirikiana kwenye Kituo cha utafiti cha mwezini
2021-06-17 10:56:54| Cri

Mamlaka za anga za mbali za China na Russia zimetangaza kwa pamoja ramani na mwongozo wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa mwezi ILRS, huku zikizialika nchi zote zinazotaka kushiriki, mashirika na wenzi wa kimataifa kushirikiana katika mradi huo.

Idara ya anga za mbali ya taifa ya China CNSA na ile ya Russia Roscosmos zimetangaza mwaliko huo mtandaoni kwenye mkutano wa uchunguzi wa anga za mbali wa dunia mwaka 2021.