Uchumi wa China waendelea kufufuka mwezi Mei
2021-06-17 08:25:24| cri

 

 

Idara ya Takwimu ya China imesema, uchumi wa China uliendelea kufufuka kwa mwelekeo mzuri katika mwezi uliopita.

Takwimu zinaonesha kuwa, mwezi Mei, ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huo, thamani inayotokana na sekta ya viwanda iliongezeka kwa asilimia 8.8, na manunuzi ya bidhaa za rejareja za matumizi yaliongezeka kwa asilimia 12, huku thamani ya jumula ya bidhaa zilizoagizwa na zilizouzwa ikiongezeka kwa asilimia 26.9.

Takwimu pia zinaonesha kuwa, sekta ya utengenezaji wa teknolojia ya juu iliongezeka kwa kasi, hasa magari yanayotumia nishati mpya.