RT: Mpango wa kundi la G7 unaolenga kushindana na pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja” ni tangazo la kisiasa tu
2021-06-18 11:06:45| Cri

Tovuti ya chombo cha habari cha Russia RT imetoa makala ikisema, mpango wa uwekezaji wa miundombinu wa kimataifa uliopendekezwa kwenye mkutano wa kilele wa G7 ambao unalenga kukabiliana na pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja” lililotolewa na China ni tangazo la kisiasa tu.

Makala hiyo iliyoandikwa na mchambuzi wa mambo ya kisiasa na uhusiano wa kimataifa wa Uingereza Bw. Tom Fowdy imesema, kwa kweli mpango huo unaoitwa mpango mbadala wa G7 hauwezi kuchukua nafasi ya mpango wowote, ambao unafaa kuchukuliwa kama tangazo la kisiasa linalosisitiza mafanikio na mvuto wa pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja” katika wakati wa kwanza.

Makala hiyo pia imesema, mvuto wa pendekezo la “Ukanda Mmoja na Njia Moja” unatokana na China kutoweka masharti ya kisiasa kwenye uwekezaji na kuziruhusu nchi nyingine kujipatia maendeleo bila kurudi nyuma kwa serikali na mashirika ya kimagharibi ambayo yalitumia mitaji ya maendeleo kulazimisha mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi.