Wachambuzi waona kuwa mfumo wa “Shule ya bweni ya Wakazi wa Asili” wa Canada ni sawa na mauaji ya kimbari
2021-06-18 10:27:21| Cri

Hivi karibuni, mabaki ya maiti za watoto 215, yamegunduliwa katika sehemu iliyokuwepo shule ya bweni ya wakazi wa asili nchini Canada. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian akizungumzia tukio hili alisema, hili ni jambo linalowasikitisha watu, na Canada sasa inapaswa kufanya  uchunguzi kwa pande zote juu ya masuala ya haki za binadamu ya nchi yake. 

Bw. Zhao Lijian ameeleza kuwa, Tume ya Ukweli na Maafikiano ya Canada imethibitisha kuwa, katika historia ya Canada, zaidi ya watoto laki 1.5 kutoka familia za wakazi wa asili nchini humo walilazimishwa kuondoka kwa wazazi wao, na kuingia katika “Shule ya bweni ya wakazi wa asili”. Akisema watoto hawa walilazimika kuacha imani zao za asili na kubadili dini na kuingia Ukristo na Ukatoliki; kulazimika kuacha lugha zao na kuongea Kiingereza na Kifaransa; kulazimika kuacha utamaduni wao wa jadi na kujifunza mila na desturi za wazungu. Watoto hao walikuwa na utapiamlo, kukosa matunzo, hata kunyanyaswa na kushambuliwa kingono.