Uwekezaji wa China kwa nchi zilizojiunga na Ukanda Mmoja na Njia Moja waongezeka
2021-06-18 09:26:19| cri

 

 

Takwimu zilizotolewa jana na Wizara ya Biashara ya China zimeonesha kuwa, kuanzia mwezi Januari hadi mwezi Mei mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja usio wa kifedha wa China kwa nchi zilizojiunga na Ukanda Mmoja na Njia Moja umefikia dola za kimarekani milioni 7,430, na kuongezeka kwa asilimia 13.8 kuliko mwaka jana wakati kama huo.

Takwimu hizo pia zimeonesha kuwa, katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, uwekezji halisi wa kigeni nchini China umefikia yuan bilioni 481, sawa na dola za kimarekani karibu bilioni 74.57, na kuongezeka kwa asilimia 35.4 kuliko mwaka jana wakati kama huu.