Katibu Mkuu wa UM atoa wito wa kuongeza muda wa kulipa madeni kwa nchi za kipato cha kati
2021-06-18 08:40:21| CRI

 

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuongeza muda wa kulipa madeni kwa nchi zilizo na kipato cha kati.

Akizungumza katika mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Umoja huo kuhusu nchi za kipato cha kati uliofanyika jana, Bw. Guterres amesema vitu vinavyohitajika kuruhusu mpangilio mpya wa ulipaji wa madeni na kupunguzwa kwa madeni hayo, vinaweza kusaidia nchi za kipato cha kati kuboresha bajeti zao ili kukuza uwekezaji na kuwa na mwelekeo mzuri na endelevu wa ufufukaji baada ya janga la virusi vya Corona.

Amesisitiza kuwa, madeni ya nchi za kipato cha kati yanapaswa kuahirishwa mpaka mwaka 2022 ili kuzipa nafasi kukabiliana na athari za kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na virusi vya Corona.