Xi Jinping asisitiza umuhimu wa kukumbuka historia ya CPC
2021-06-19 21:44:09| cri
Xi Jinping asisitiza umuhimu wa kukumbuka historia ya CPC
Rais Xi Jinping wa China ametembelea Jumba la Makumbusho la Historia ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akisisitiza umuhimu wa kukumbuka historia ya Chama hicho.
Rais Xi ametembelea jumba hilo wakati China inapoadhimisha kutimia kwa miaka 100 tangu kuanzishwa kwa CPC. Ameagiza kujifunza, na kujumisha vizuri historia ya chama hicho, kurithisha na kueneza uzoefu wenye thamani kubwa wa chama hicho, na kupata nguvu ya kusonga mbele kupitia historia ya chama hicho.