Marekani yaandaa vikwazo vipya dhidi ya Russia kufuatia suala la Navalny
2021-06-21 07:57:11| Cri

Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jake Sullivan amesema, nchi hiyo inapanga kuweka vizuizi vingine dhidi ya Russia kwa tuhuma za kumlisha sumu mkosoaji wa serikali ya nchi hiyo, Alexei Navalny.

Sullivan amesema hayo katika mahojiano na kituo cha habari cha CNN cha Marekani, alipojibu swali kama serikali ya Marekani itaongeza shinikizo dhidi ya Russia juu ya suala hilo.

Ameongeza kuwa, vikwazo hivyo vitawekwa mapema mara baada ya maandalizi ili kuhakikisha wanatimiza malengo sahihi, na kwamba wataweka vikwazo zaidi kwa silaha za kemikali.

Sullivan alisema hayo baada ya rais wa Marekani Joe Biden kukutana na mwenzake wa Russia Vladimir Putin huko Geneva, Uswizi, ukiwa ni mkutano wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu Biden aingie madarakani.