China yatoa chanjo bilioni 1 za COVID-19 kwa wananchi wake
2021-06-21 08:07:47| Cri

Kamati ya Afya ya China (NHC) imesema, zaidi dozi bilioni moja za chanjo ya virusi vya Corona zimetolewa nchini China mpaka kufikia Jumamosi iliyopita, huku nchi hiyo ikiendelea na zoezi kubwa la utoaji wa chanjo katika historia yake.

Naibu mkuu wa Kamati hiyo Zeng Yixin amesema, kuanzia mwishoni mwa mwezi Machi, China imeongeza kasi ya utoaji bure wa chanjo ya virusi vya Corona kwa nchi nzima, na imechukua siku 25 kufikia dozi milioni 200 kutoka dozi milioni 100, siku 16 kufikia dozi milioni 300, na siku zita kufikia dozi milioni 900.

Amesema, kampeni kubwa ya utoaji wa chanjo inayofanyika nchini China imeonyesha kuwa, chanjo za virusi vya Corona za nchini China ni salama.

Jumla ya chanjo 21 za virusi vya Corona zimeingia kwenye majaribio ya kliniki nchini China kuanzia mwaka jana, na mpaka sasa, chanjo nne zimepewa masharti ya kuingia kwenye soko, na tatu zimepewa idhini ya kutumika kwa dharura ndani ya nchi.