Balozi wa Marekani kurudi Moscow wiki hii
2021-06-22 09:01:41| Cri

Balozi wa Marekani nchini Russia John Sullivan atarejea Moscow wiki hii.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price amesema Marekani inafuata ahadi yake ya kuwepo kwa njia wazi za mawasiliano na serikali ya Russia, ikiwa ni juhudi ya kukuza maslahi ya Marekani, lakini pia kupunguza hatari zinazoweza kusababishwa na maelewano mabaya kati ya nchi hizi mbili.

Pia amesema balozi wa Russia nchini Marekani Anatoly Antonov tayari amerudi Washington.

Mvutano uliongezeka kati ya Marekani na Russia mapema mwaka huu. Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilimwita nyumbani balozi Antonov mwezi Machi ili kufanya majadiliano ya ngazi ya juu, na Sullivan aliondoka Russia kwa sababu zinazofanana mwezi Aprili.