Rais mteule wa Iran asema Marekani inatakiwa kuondoa vikwazo vyote
2021-06-22 08:59:14| Cri

Rais mteule wa Iran Ebrahim Raisi amesema, Marekani inatakiwa kuondoa vikwazo vyote dhidi ya Iran, na nchi za Ulaya kufuata ahadi zao bila ya kutii shinikizo na sera za nje za Marekani kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

Raisi amesema hayo kwenye mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari baada ya kuchaguliwa. Pia amesema Iran haitajadili sera zake za kikanda wala mpango wa makombora na nchi za nje.

Alipoulizwa kama yupo tayari kukuana na rais Joe Biden wa Marekani ikiwa vikwazo vyote vitaondolewa na mahitaji yote ya Iran kukidhiwa, Raisi alisema hayuko tayari.