Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa atoa wito wa kufuatilia kwa makini hali nchini Afghanistan
2021-06-23 09:05:05| Cri

Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Zhang Jun ameeleza ufuatiliaji mkubwa juu ya hali nchini Afghanistan na kuiomba jamii ya kimataifa kusaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Balozi Zhang amesema hali ya sasa nchini Afghanistan imefikia katika hatua muhimu ya njia panda, na nchi hiyo imeingia kwenye kipindi kipya cha kukosa utulivu. Amesema tangu Marekani itangaze kuondoa vikosi vyake katikati ya mwezi Aprili, mazungumzo ya ndani ya Afghanistan yamerudi nyuma badala ya kusonga mbele, na hali ya kiusalama, kiuchumi na kibinadamu inazorota.

Ameliambia Baraza la Usalama kuwa ni muhimu kufikiria kwa makini chanzo cha hali ya sasa nchini Afghanistan, na ni kitu gani kitaweza kuleta utulivu na usalama wa kudumu nchini humo katika siku zijazo.