China yazitaka nchi husika kushughulikia ukiukaji mbaya wa haki za binadamu
2021-06-23 08:01:27| Cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema, China imezitaka nchi husika kuchukua hatua madhubuti kushughulikia matatizo yao makubwa ya haki za binadamu.

Kauli hiyo imekuja baada ya taarifa ya pamoja iliyotolewa na nchi 65 katika Mkutano wa 47 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC) kuunga mkono msimamo wa China, na kupinga kuingilia mambo ya ndani ya China kwa kisingizio cha haki za binadamu.

Wakati Canada, kwa niaba ya baadhi ya nchi za magharibi, ikishambulia na kuishutumu China juu ya masuala yanayohusiana na Xinjiang, Hong Kong, na Tibet, nchi hizo 65 zimezihimiza Canada na nchi nyingine za magharibi kufuata madhumuni na kanuni za mkataba wa Umoja wa Mataifa, kupinga kuyafanya masuala ya haki za binadamu kuwa ya kisiasa, kutumia vigezo viwili, na kutoa tuhuma zisizo na msingi zinazotokana na malengo ya kisiasa dhidi ya China.