China yaitaka Marekani kusimamisha vikwazo vya upande mmoja dhidi ya nchi nyingine
2021-06-24 08:34:21| Cri

Mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ameitaka Marekani kusimamisha vikwazo vya upande mmoja dhidi ya nchi nyingine.

Balozi Zhang amesema hayo katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa alipozungumzia umuhimu wa kumaliza vikwazo vya kiuchumi, kibiashara, na kifedha vilivyowekewa na Marekani dhidi ya Cuba.

Amesema vizuizi dhidi ya Cuba na hatua za kulazimisha dhidi ya nchi nyingine haziendani na mwelekeo wa amani wa kimataifa, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana. Ameongeza kuwa, hatua hizo zinakiuka makubaliano ya kimataifa juu ya Ajenda ya 2030 na kudhuru haki za watu wa nchi husika za kuishi na kupata maendeleo, na haki za kimsingi za binadamu.