Balozi wa Somalia nchini China asifu maendeleo yaliyopatikana katika mkoa wa Xinjiang
2021-06-24 09:18:07| Cri

Balozi wa Somalia nchini China asifu maendeleo yaliyopatikana katika mkoa wa Xinjiang_fororder_索马里驻华大使

Balozi wa Somalia nchini China Awale Ali Kullane amesifu maendeleo yaliyopatikana katika mkoa wa Xinjiang nchini China.

Akizungumza na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG), Balozi Kullane amesema, katika ziara yake mkoani humo, alishuhudia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika sekta mbalimbali ikiwemo ujenzi wa miundombinu, na kilimo.

Amesema tofauti na ripoti zinazotolewa kwenye vyombo vya habari vya nchi za Magharibi, wakazi wa mkoa wa Xinjiang wanaishi kwa amani na masikilizano, na wanafanya kazi kwa pamoja ili kuondokana na umasikini.