Watoto 1,245 katika wilaya ya Lasanimu, Tibet, China wamepata elimu bure ya awali kabla ya chekechea
2021-06-24 14:39:39| cri

Mpango wa elimu ya awali kabla ya chekechea katika familia za vijijini umezinduliwa Mfuko wa utafiti wa maendeleo wa China katika wilaya ya Qixingguan mkoa wa Guizhou, wilaya ya Huachi mkoani Gansu na wilaya ya Jimunai mkoani Xinjiang.

Kuanzia mwaka 2018, wilaya ya Nimu mkoani Tibet pia imechaguliwa kuwa kituo cha majaribio ya mpango huo, na hivi sasa mpango huo umeajiri wasimamizi wakuu wawili, wasimamizi 16 wa manispaa na wilaya na walimu 114, na kuwanufaisha watoto 1,245 katika wilaya hiyo.

Utafiti husika umethibitisha kuwa, kuwekeza katika maendeleo ya mapema ya watoto ni njia ya msingi ya kuondokana na umaskini. Mpango huo unalenga kutoa elimu inayowafaa watoto wa kuanzia miezi 6 hadi 26, ili kutafuta njia yenye ufanisi ya kuondoa mizizi ya umaskini vijijini.

Katika mpango huo, walimu wanaenda nyumbani kwa familia za watoto hao na kucheza nao, kuwafundisha nyimbo za watoto, kufahamu hali ya mwili, chakula na mawasiliano kati ya walezi wa watoto, ili kuweka rekodi na kutoa ushauri.