Kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma ndio msingi wa CPC kukubalika na kupendwa na wananchi
2021-06-24 08:48:22| cri

Kutoa kipaumbele kwa maslahi ya umma ndio msingi wa CPC kukubalika na kupendwa na wananchi_fororder_坦桑尼亚驻华大使

Ripoti moja iliyotolewa Julai 2020 na Chuo Kikuu cha Harvard cha Marekani yenye jina "Understanding the Resilience of the Chinese Communist Party: A Long-term Survey of Chinese Public Opinion", inasema tofauti na vyama vingine vya kikomunisti duniani, mvuto wa chama cha Kikomunisti cha China umeendelea kuongezeka na uungaji mkono wake umefikia asilimia 93%.

 

Kumekuwa na maswali kwanini CPC imeendelea kuwa na mvuto na kuwa na uungaji mkono mkubwa kutoka kwa umma? Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki, amesema sababu kubwa inayofanya chama cha kikomunisti kubwa ni kuwa CPC ni chama cha watu na imekuwa ikijishughulisha na maswala ya watu. Na wakati wote kimekuwa kikijibadilisha kulingana na mahitaji ya wakati na mahitaji ya watu. Siku zote chama cha siasa kazi yake ni kuhudumia wananchi na kuwafanya watu wawe na furaha, na kuhakikisha watu wanapata huduma za msingi kama maji, chakula, nguo, umeme na mahitaji yote ya kimsingi. Chama cha kikomunisti kimekuwa kinajitadi kuhakikisha mahitaji ya watu yanapatikana kwa wakati wote. Hakijawa chama kinachokataa mabadiliko, kimekuwa kinabadilika kutokana na mahitaji ya wakati.

Mfano mzuri wa mabadiliko ni utekelezaji wa sera ya mageuzi kufungua milango. Kutokana na CPC kutekeleza sera hiyo tumeona uwekezaji kutoka nje ulivyoleta mabadiliko mbalimbali. Kwa hiyo kama wananchi wanaona maisha yao yanaboreka, mapato yao yanaongezeka, wanakuwa na ziada ya pesa kwa ajili ya utalii na mapumziko yao na familia zao, bila shaka watakuwa na imani na chama. Kwa kuwa wanajua hiki ndio chama kilichowaletea neema hiyo. Kama unaona vyama vingine vimepoteza uungaji mkono, basi ni kwa sababu vimepoteza muunganiko na wananchi. Labda viongozi wa vyama hivyo walilewa madaraka wakaanza kushughulikia mambo yao binafsi na utajiri wao binafsi, wakaachaa kushughulikia mambo ya msingi ya wananchi, kwa hiyo wananchi wakakasirika na kuchagua vyama vingine. Lakini hapa China CPC haikuwa hiyo, imeendelea kuzingatia maslahi ya wananchi. Tunaona hata vyama vingine nje ya China ambavyo vinafuata mfano kama wa CPC. Kwa mfano chama cha CCM cha Tanzania, ni chama kinachofuata mfano wa CPC kwa kutoa kipaumbele kujishughulisha na maswala ya watu, kama maji, elimu, miundombinu, na ndio maana mpaka sasa bado viko madarakani.