Filamu mbili za katuni za kuadhimisha miaka 100 ya CPC zilizotengenezwa na CMG zatolewa rasmi
2021-06-24 15:57:29| cri

Katika kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), filamu mbili za katuni zilizotengenezwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) zilionyeshwa rasmi jana Juni 23. Hafla ya kusaini makubaliano ya ushirikiano kati ya CMG na idara husika za mji wa Beijing kuhusu katuni za watoto pia ilifanyika siku hiyo.

Naibu mkurugenzi wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC na mkurugenzi mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong alihudhuria na kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano husika.