Mtu wa pili katika timu ya Olimpiki ya Uganda athibitishwa kuwa na virusi vya Corona nchini Japan
2021-06-25 09:17:33| Cri

Kamati ya Olimpiki ya Uganda imethibitisha kuwa, mtu wa pili katika timu ya Uganda amegunduliwa kuwa na virusi vya Corona nchini Japan.

Wikiendi iliyopita wakati kundi la kwanza la ujumbe wa Uganda lenye watu tisa lilipofika Japan kwa ajili ya mazoezi kabla ya mashindano ya Michezo ya Olimpiki, kocha mmoja aligunduliwa kuwa na virusi vya Corona na kutengwa mjini Tokyo. Watu wengine wa timu hiyo waliruhusiwa kwenda kwenye kambi ya mafunzo mjini Izumisano, lakini pia walitengwa.