Chama cha CPC chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping kimefanya kazi kubwa katika kupambana na umaskini
2021-06-25 08:35:03| cri

Chama cha CPC chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping kimefanya kazi kubwa katika kupambana na umaskini_fororder_坦桑尼亚驻华大使

Chama cha Kikomunisti cha China (CPC)kinafanya maadhimisho ya miaka 100 tangu kianzishwe huku kikiwa kimetimiza malengo makubwa ya kuendeleza taifa, na kuwaondoa watu wake kutoka kwenye lindi la umaskini. Lakini wakati China inafurahia mafanikio hayo, uongozi wa CPC na mchango wa katibu mkuu Bw. Xi Jinping ni msingi mkuu wa mafanikio hayo.

 

Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki, amesema ili kujua vizuri China imeweza vipi kutokomeza umaskini, tunatakiwa kuangalia jinsi CPC ilivyoweka mipango madhubuti ya kupambana na umaskini. Na baada ya kuweka mipango hiyo, CPC iliwaieleza vizuri makada wa chama ambo ni watekelezaji wa mipango hiyo, lakini pia iliwaeleza wananchi wanaotakiwa kuondolewa kwenye umaskini kuhusu mipango hiyo.

 

Lakini jambo lingine muhimu ni kuwa, CPC imesimamia vizuri na kwa makini utekelezaji wa mipango hiyo katika ngazi zote, kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya shina. Sisi tukioko hapa China ni mashahidi, na mara kwa mara hatukosi kuona katibu mkuu wa chama Bw. Xi Jinping yeye mwenyewe akienda kwenye ngazi ya chini kabisa (ngazi ya shina) kuonana na wananchi maskini na kukagua utekelezaji wa mipango ya kupambana na umaskini katika maeneo yao.

 

Yeye akiwa kiongozi mkuu wa chama akiendea kufanya ukaguzi kwenye ngazi ya chini kabisa, ina maana viongozi wote wa chama cha ngazi ya mikoa, wilaya, kata, tarafa, hadi kijiji pia wanakwenda kufanya ukaguzi kuhakiakisha mipango ya kupambana na umaskini inatekelezwa. Na viongozi wa chama huwa wanafanyiwa tathmini kujua wamefanya nini kwenye utekelezaji wa kazi ya kupambana na umaskini. Hata katibu mkuu wa sasa Bw. Xi Jinping, yeye mwenyewe alipokuwa katibu wa chama wa mkoa wa Fujian, aliwahi kukaguliwa kuhusu mchango aliotoa katika kupambana na umaskini. Kwa hiyo uongozi bora wenye kuona mbali, kuweka mipango ya kuondoa umaskini, na kusimamia utekelezaji wa mipango hiyo, imekuwa sifa ya kipekee ya CPC kupambana na umaskini chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping.