China yafuatilia ukiukaji wa haki za binadamu wa baadhi ya nchi za magharibi dhidi ya wahamiaji
2021-06-25 08:17:09| Cri

Balozi wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Jiang Duan amesema, China inafuatilia sana ukiukaji wa haki za wahamiaji na wakimbizi katika baadhi ya nchi na sehemu, zikiwa ni pamoja na Marekani, Umoja wa Ulaya, Uingereza, Australia na Canada.

Balozi Jiang amesema hayo katika taarifa iliyowasilishwa Jumatano katika Mkutano wa 47 wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, akisema baadhi ya nchi zinawashikilia wahamiaji katika vituo vya wahamiaji chini ya mazingira mabaya kwa muda mrefu. 

Balozi Jiang amesema, baadhi ya nchi zinawashikilia wahamiaji katika vituo vilivyoko baharini, ambapo wahamiaji wananyanyaswa, na katika baadhi ya nchi, vituo hivyo vinaendeshwa na mashirika ya watu binafsi, ambapo matukio ya unyanyasaji na matumizi mabaya ya nguvu yanatokea mara kwa mara, na haki za binadamu za wahamiaji zinakiukwa.