China yatoa waraka mweupe kuhusu jinsi CPC inavyotekeleza ulinzi wa haki za binadamu
2021-06-25 08:22:48| Cri

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka mweupe kuhusu hatua za Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kinavyoheshimu na kulinda haki za binadamu.

Waraka huo umesema, huu ni mwaka wa 100 tangu kuanzishwa kwa CPC, na katika mwongo uliopita, Chama hicho kimewekeza juhudi kubwa katika ulinzi wa haki za binadamu, na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya haki za binadamu duniani.

Kwa mujibu wa waraka huo, chini ya uongozi wa CPC na kutokana na msingi wa Katiba, mfumo wa ujamaa wa China umeundwa na kutoa utaratibu kamili wa kisheria ili kulinda haki za binadamu.

Aidha, waraka huo umesema China imeshiriki kikamilifu katika masuala ya haki za binadamu ya kimataifa, ikitoa mchango wake katika usimamizi na maendeleo ya haki za binadamu duniani, na kufanya kazi pamoja na nchi nyingine kuunda jamii ya kimataifa ya binadamu yenye hatma ya pamoja.