Marekani yasema bado kuna tofauti ya maoni kuhusu masuala makubwa kwenye mazungumzo juu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran
2021-06-25 09:18:18| Cri

Ofisa mwandamizi wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema, baada ya duru ya sita ya mazungumzo, nchi hiyo na Iran bado zina tofauti kubwa juu ya masuala muhimu katika kurejesha makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 (JCPOA).

Kuanzia mwezi Aprili mwaka huu, Marekani na Iran zimefanya duru sita za mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Vienna nchini Austria, ili kurejesha makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Ofisa huyo amesema, bado kuna masuala makubwa kati ya pande zote mbili yatakayohitaji kutatuliwa. Pia amesema bado kuna uwezekano wa kufikia makubaliano kati ya nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa ujumbe wa Marekani utashiriki kwenye duru ya saba ya mazungumzo hayo itakayofanyika katika siku za karibuni.