Ofisi ya siasa ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC imefanya mafunzo ya 31 ya pamoja. Mafunzo hayo yamefanywa kwa mtindo wa matembezi na mjadala. Viongozi wa chama na serikali akiwemo Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Wang Huning, Zhao Leji na Hanzheng wametembelea makazi ya zamani ya rais wa zamani wa China Marehemu Mao Zedong.