Vyombo vya habari vya Afrika vyaiandikia barua CMG kupongeza maadhimisho ya miaka 100 ya CPC
2021-06-28 17:04:09| cri

Vyombo vingi vya habari vya Afrika vyaiandikia barua CMG kupongeza maadhimisho ya miaka 100 ya CPC_fororder_微信图片_20210628160500

Wakuu wa vyombo vingi vya habari vya nchi za Afrika wamemwandikia barua naibu mkuu wa idara ya uenezi ya kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na mkuu wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG Bw. Shen Haixiong kupongeza maadhimisho ya miaka 100 ya kuanzishwa kwa CPC.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyombo vya Habari la Kenya MCK Maina Muiruri,amesema “tumeshuhudia kuwa katika karne iliyopita haswa katika miongo minne iliyopita, China imepata maendeleo makubwa katika sekta za siasa, jamii na uchumi. Maendeleo hayo yametia moyo na kusisimua watu.”

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji la Kenya Dkt. Naim Bilal amesema “kwa kutumia fursa hii ya maadhimisho ya miaka 100 ya CPC, napongeza Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na kutarajia kuimarisha ushirikiano zaidi na CMG.”

Na mhariri mkuu wa shirika la habari la Sudan SUNA Mohamed Osman Adam amesema “Sudan na China na wananchi wao tuna uhusiano thabiti wa kirafiki. Shirika la habari la Sudan limeshuhudia mafanikio makubwa iliyopata China, na pia kushuhudia jinsi wananchi wa nchi hizo mbili wanavyojitahidi bega kwa bega kujenga siku nzuri za baadaye.”

Bw. Shen Haixiong alijibu barua mtawalia kwa vyombo vya habari. Kwenye barua hizi amesema kutokana na uongozi imara wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China chini ya katibu mkuu Xi Jinping, watu wa China wako katika safari za kutafuta ustawishwaji wa taifa. Amesema CMG itashirikiana na vyombo vya habari vya nchi mbalimbali, kutafuta maoni ya pamoja, kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano na kuchangia busara na nguvu kwenye kujenga utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na sahihi na jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.