Ukraine yatangaza kujitoa kwenye “Taaria ya Pamoja kuhusu Haki za Binadamu za Xinjiang”
2021-06-28 11:09:44| cri

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ukraine tarehe 24 ilitoa taarifa ikisisitiza kuwa nchi hiyo inazingatia uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati yake na China, na tarehe 25 ilitangaza kufuta uamuzi wake wa kusaini “Taarifa ya Pamoja kuhusu Haki za Binadamu za Xinjiang” iliyoanzishwa katika Mkutano wa 47 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo pia inasisitiza kuwa Ukraine haiingilii kati mambo ya ndani ya China, na kupenda kuendelea kufuata kanuni za kuheshimiana uhuru, mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kujitahidi kuhimiza uhusiano kati yake na China kupata maendeleo mapya.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China tarehe 26 akijibu maswali kuhusu hatua hiyo ya Ukraine alisema, uamuzi wa Ukraine umeonesha  uhuru wake wa kujiamulia na nia yake ya kuheshimu ukweli wa mambo, hali ambayo inafuata katiba ya Umoja wa Mataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, ambayo China inaikaribisha.