Marekani yashambulia vifaa vya wapiganaji wanaoungwa mkono na Iran nchini Iraq na Syria
2021-06-28 09:38:22| CRI

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema Marekani imefanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo vinavyotumiwa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika eneo la mpaka kati ya Iraq na Syria.

Wizara hiyo ilitoa taarifa kuwa Marekani ilishambulia maghala ya silaha katika maeneo mawili nchini Syria na eneo moja nchini Iraq karibu na mpaka kati ya nchi hizo.

Marekani imechagua shabaha hizo kwa sababu maghala hayo yanatumiwa na wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran ambao wanahusika na mashambulizi ya kutumia droni (UAV) dhidi ya wafanyakazi na vifaa vya Marekani nchini Iraq.