Xi Jinping asisitiza kuwepo na mafanikio mapya kufuatia maadhimisho ya miaka 100 ya CPC
2021-06-28 14:49:56| cri

 

 

Kufuatia maadhimisho ya miaka 100 ya kuasisiwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC, amesisitiza kufanya juhudi za kuleta mafanikio mapya ambayo yatahimili majaribu ya wakati na yatakayokuwa na tija kwa watu.

Rais Xi ameyasema hayo siku ya Ijumaa wakati akihutubia kikao cha  timu ya utafiti ya Ofisi ya Siasa ya Kamati ya Kuu ya CPC. Baada ya kutembelea jengo lenye umuhimu mkubwa katika historia ya chama, rais Xi ametoa wito wa kuelewa kwa kina sheria inayosimamia maendeleo ya historia ya jamii ya binadamu yenye nadharia ya Umaksi

Ametilia mkazo kuwa inapaswa kufanywa juhudi ya kuelimisha na kuongoza wajumbe na maafisa wa chama ili wawe wakweli kwenye nia ya asili na kazi ya awali ya Chama, na kufuata filosofia ya maendeleo ya watu na kufanya kazi bila kusita kwa ajili ya kuhuisha zaidi taifa la China.