Mjumbe wa China akosoa uhalifu wa mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi
2021-06-29 08:50:29| CRI

Mwanadiplomasia mwandamizi wa China amekosoa uhalifu wa mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi, akiihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya uchunguzi wa kina, wa pande zote na bila upendeleo kuhusu uhalifu wote wa mauaji ya kimbari, na kutokomeza ubaguzi wa rangi na matatizo yaliyosalia ya mauaji ya kimbari.

Akiongea kwenye Mazungumzo na Mshauri Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kuzuia Mauaji ya Kimbari, konsela wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Mataifa mjini Geneva Bw. Jiang Duan, amesema mauaji ya kimbari ni uhalifu mkubwa wa kimataifa usiokubalika kwa pande zote na athari za uhalifu huo bado zipo hadi leo.

Bw. Jiang amesema, Wakazi wa asili wa Marekani walifukuzwa kutoka kwenye ardhi zao na kuchinjwa kwenye kipindi wanachokiita “Upanuzi wa Kuelekea Magharibi” katika karibu miaka mia moja baada ya nchi hiyo kuanzishwa. Idadi ya watu hao ilipungua kutoka milioni 5 ya karne ya 15 hadi kufikia laki 2.5 ya mwanzoni mwa karne ya 20.

Bw. Jiang amebaini kuwa nchini Canada, zaidi ya watoto laki 1.5 wa wakazi wa asili walilazimishwa kwenda katika shule za bweni, na watoto wasiopungua 3,200 kati yao walidhalilishwa hadi kufa.

Pia amesema nchi nyingine za Magharibi pia zilitenda uhalifu mkubwa wa mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu wakati wa ukoloni na kuvamia nchi nyingine.