China yafanya maonesho ya sanaa kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 ya CPC
2021-06-29 09:25:15| CRI

Maonesho ya sanaa yamefanyika mjini Beijing kusherehekea maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC).

Viongozi wa chama na serikali ya China rais Xi Jinping, Bw. Li Keqiang, Bw. Li Zhanshu, Bw. Wang Yang, Bw. Wang Huning, Bw.Zhao Leji, Bw. Han Zheng na Bw. Wang Qishan pamoja na watu wapatao 20,000 walitazama maonyesho hayo yaitwayo "Safari Kuu," kwenye uwanja wa  michezo wa kitaifa.

Maonesho hayo yalizinduliwa kwa kurusha fataki inayoonesha nambari 100 kwenye anga ya uwanja huo. Maonyesho yaligawanywa katika sehemu nne, ambazo zimeonyesha jinsi watu wa China walivyofanya mapinduzi, ujenzi na mageuzi chini ya uongozi wa CPC katika miaka 100 iliyopita.